Saturday, February 11, 2017

VPL: SIMBA 3 VS 0 TANZANIA PRISONS, SIMBA HUYOO KILELENI!

Simba Leo wamekaa kileleni mwa VPL, Ligi Kuu Vodacom, baada ya kuichapa Tanzania Prisons 3-0 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Simba sasa wana Pointi 51 kwa Mechi 22 wakifuata Mabingwa Watetezi Yanga wenye Pointi 49 kwa Mechi 21.
Katika Mechi ya Leo, Simba waliongoza 2-0 hadi Mapumziko kwa Bao za Juma Luizio na Ibrahim Ajib .
Simba walipiga Bao la 3 Dakika ya 67 Mfungaji akiwa Laudit Mavugo.
Jumapili zipo Mechi 3 za VPL na Mwadui FC itacheza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Mwadui wakati African Lyon itacheza na Mtibwa Sugar Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na pia JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Mbao FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

VIKOSI:
SIMBA:
Daniel Agyei, Janvier Bokongu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Method Mwanjali [Mwinyi Kazimoto, 62’], James Kotei, Said Ndemla, Muzamil Yassin, Laudit Mavugo, Ibrahim Ajib [Pastory Athanas, 74’], Juma Luizio [Shiza Kichuya, 70’]

PRISONS:
Laurian Mpalile, Aaron Kalambo, Salum Kimenya, James Mwasote, Nurdin Chona, Jumanne Elfadhil, Lambert Sibiyanka, Kazungu Nchinjayi Kassim Hamisi, 38’], Victor Hangaya [Salum Bosco, 76’], Mohammed Samatta na Benjamin Asukile [Meshack Suleiman, 56’]
REFA: Alex Mahagi [Mwanza]
 

VPL – Ligi Kuu Vodacom
Ratiba
Jumapili Februari 12

Mwadui vs Mbeya City
African Lyon vs Mtibwa Sugar
JKT Ruvu vs Mbao FC


VPL – Ligi Kuu Vodacom
Matokeo:
Jumamosi Februari 11

Simba 3 Tanzania Prisons 0
Stand United 0 Majimaji 0
Ndanda FC 0 Toto African 0
Ruvu Shooting 0 Azam FC 0