Thursday, February 23, 2017

VPL...JUMAMOSI – SIMBA v YANGA, TIKETI ZADAIWA KUADIMIKA, NANI ATAIBUKA KIDEDEA?

JUMAMOSI Februari 25, Barabara na vichochoro vyote vitaelekea Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kushuhudia mtanange kati ya Vigogo Wawili Nchini, Simba na Yanga, wakipambana kwenye Mechi ya VPL, Ligi Kuu Vodacom.

Mbali ya hii kuwa Dabi, kihalali inapaswa kuitwa Dabi yay a Kariakoo kutokana na ukweli Timu zote ni za Kitongoji cha Kariakoo Jijini Dar, Mechi hi inakutanisha Mahasimu hawa wakiwa wao Wawili ndio pekee wamo kwenye mbio kali na halisi za Ubingwa wa Tanzania Bara Msimu huu.

VPL, inayoshirikisha Timu 16, sasa inaongozwa na Simba wenye Pointi 51 kwa Mechi 22 na Yanga ni wa Pili wakiwa na Pointi 49 kwa Mechi 21 huku Azam FC ni wa 3 wakiwa na Pointi 41 kwa Mechi 23.

Simba, chini ya Kocha kutoka Cameroun, Joseph Omog, akisaidiwa na Mganda Jackson Mayanja, wamepiga Kambi huko Zanzibar wakati Yanga, chini ya Kocha Mkuu George Lwandamina, anaesaidiwa na Juma Mwambusi, wako huko Kigamboni, eneo la Kimbiji, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam.

Kambi zote mbili zimekuwa ‘bubu’ kuzungumzia hali halisi za Vikosi vyao, hasusan Wachezaji walioripotiwa Majeruhi, n azote zimesisitiza umuhimu wa Bigi Mechi hii na kujipa moyo wa ushindi.


UWANJA WA TAIFA, DAR ES SALAAM
VIINGILIO:

-VIP A 30000
-VIP B NA C 20,000
-ORANGE 10,000
-KIJANI NA BLUE 7000


Mbali ya Timu husika kuhaha kwa matayarisho ya mtanange huu, Washabiki pia wamekuwa kwenye pilikapilka za kununua Tiketi mapema kupitia MaxMalipo lakini ripoti zimezagaa kuwa Tiketi hizo zimeanza kuadimika baada ya kununuliwa kwa wingi mapema mno.
Tiketi ambazo zimedaiwa kuadimika mno ni zile za Bei ya chini, Shilingi 7,000 na 10,000, na ipo dhana zitaibuka mikononi mwa Watu baki Ijumaa na Siku ya Mechi Jumamosi zikiuzwa kwa Bei ya juu.
VPL – Ligi Kuu Vodacom
Msimamo
Kwa Hisani ya Soka_APP
Ratiba
Jumamosi Februari 25

Simba v Yanga

Jumamosi Machi 4
Simba v Mbeya City
Ndanda FC v Ruvu Shooting
Toto African v Mbao FC
Azam FC v Stand United
Kagera Sugar v Maji Maji FC

Jumapili Machi 5
Mtibwa Sugar v Yanga
African Lyon v Mwadui FC