Sunday, March 19, 2017

ARSENE WENGER KUTANGAZA HATIMA YAKE HIVI KARIBUNI!

Harry Redknapp expects Arsene Wenger to end his 21-year tenure with Arsenal this summerMeneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa atatamka kuhusu hatima yake hivi karibuni baada ya kufikia uamuzi kama atabaki Arsenal au la.
Wenger alizungumza hayo Jana mara baada ya kutwangwa 3-1 na West Bromwich Albion huko The Hawthorns katika Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, hicho kikiwa ni kipigo chao cha 4 katika Mechi 5 za EPL kina kilichowatupa Nafasi ya 5 na kuhatarisha kumaliza kwao ndani ya 4 Bora kitu ambacho hakijawakuta tangu 1996.
Kipigo hicho kimeongeza presha kwa Wenger huku Mashabiki wengi wakitaka ang’oke kwenye Klabu hiyo ambayo yupo tangu 1996.

Arsenal fans held up banners calling for Wenger to leave at the end of the current seasonWenger ameeleza: “Ninajua nitakachofanya. Nyie mtajua hivi karibuni!”
Wenger, mwenye Miaka 67, aliongeza: “Leo sina wasiwasi na kipigo hiki. Kwa sasa tupo katika kipindi kibaya kupita chochote kwa Miaka 20! Tunafungwa Gemu baada ya Gemu na hilo kwangu ni muhimu kuliko hatima yangu!”

Mkataba wa Wenger unamalizika mwishoni huu na arsenal ishampa Ofa ya Mkataba Mpya wa Miaka Miwili.

Alan Shearer, Lejendari wa England, akiongea na BBC, Shirika la Utangazaji la BBC:

“Matamshi yake yanaonyesha ataondoka. Anaonekana kama Mtu alievunjika Moyo. Mitandaoni Watu wameongea mengi. Lakini Wachezaji wake hawajaongea lolote. Leo wameongea. Uchezaji wao unaonyesha hawamtaki Wenger. Uwanjani hawana Mioyo, hawapigani, hawana mwelekeo. Ukimwondoa Alexis Sanchez, wengine wote ni fedheha tupu!