Monday, March 13, 2017

EMIRATES FA CUP – TATHMINI – LEO VINARA WA LIGI CHELSEA vs MANCHESTER UNITED

JUMATATU Usiku Jose Mourinho anarejea tena Stamford Bridge Jijini London kwa mara ya Pili akiwa Meneja wa Manchester United kuiongoza Timu yake hiyo kuikwaa Timu yake ya zamani Chelsea kwenye Mechi ya Robo Fainali ya FA CUP ambayo wao ndio Mabingwa Watetezi.
Safari hii jambo jipya kwa Mechi hii ya Mashindano haya ni kuwa kuanzia Hatua hii ya Robo Fainali hamna tena Marudiano ikiwa Timu zitatoka Sare katika Dakika 90 na hivyo upo uwezekana wa Mechi kwenda Dakika za Nyongeza 30 na pia kupigwa Mikwaju ya Penati Tano Tano ili tu kupata Mshindi hiyo hiyo Jumatatu Usiku.

Vile vile, mabadiliko mengine ni kuwa kila Timu ipo ruksa kuingiza Mchezaji wa Nne kutoka Benchi ikiwa tu Mechi hiyo itafikia Dakika za Nyongeza 30.

Mechi kwa hii kwa Man United hasa tu kwa vile Alhamisi Usiku walikuwa huko Urusi kucheza na FC Rostov katika Mechi ya UEFA EUROPA LIGI na sasa wamesafiri tena kwenda Jijini London.

Vile vile, mara ya mwisho kwa Timu hizi kukutana Chelsea iliitwanga Man United 4-0 kwenye Mechi ya Ligi lakini tangu wakati huo Man United wameselelea kwenye wimbi la kutofungwa kwenye Ligi hata mara moja.
Kwa Chelsea, tangu wafungwe na Tottenham katika Mechi yao ya kwanza ya Mwaka 2017 hawajafungwa tena katika Mechi 10 na pia tangu Meneja wao Antonio Conte aanze kibarua wamefungwa mara 1 tu Uwanjani kwao Stamford Bridge na hiyo ilikuwa ni Septemba walipocheza na Liverpool.

Kwenye FA CUP, Man United na Chelsea zimevaana mara 13 na Man United kushinda mara 8, Sare 2 na Kufungwa 3.

Kila Timu inatarajiwa kuwa na Kikosi chao kamili lakini Man United wana pigo kubwa la kumkosa Mfungaji wao Bora Zlatan Ibrahimovic ambae ataanza Kifungo cha Mechi 3 kuanzia Mechi hii.
Tegemezi kubwa la Chelsea na tishio lao kubwa ni Mafowadi wao Eden Hazard na Diego Costa huku Kiungo wao N'Golo Kante ndio Kiungo Mkabaji wao akisimama imara kuilima Difensi yao ya Mtu 3 kwenye Mfumo wao 3-4-3 ambao umewapa mafanikio makubwa tangu wauanze walipocharazwa 3-0 Mwezi Septemba Mwaka Jana.

Mshindi wa Mechi hii ataungana na Man City, Arsenal na Tottenham ambazo tayari zimetinga Nusu Fainali na Droo ya kupanga Mechi hizo za Nusu Fainali itafanywa Jumatatu Usiku mara baada ya kumalizika kwa Mechi kati ya Chelsea na Man United.
Mechi za Nusu Fainali zote zitafanyika Uwanjani Wembley Jijini London hapo Aprili 22 na 23.

Uso kwa Uso:
Ushindi:

-Chelsea 44 Man United 59 Sare 46