Thursday, March 16, 2017

ENGLAND: JERMAIN DEFOE, MARCUS RASHFORD, JAKE LIVERMORE, LUKE SHAW NDANI YA KIKOSI CHA GARETH SOUTHGATE

Gareth Southgate Leo ameshangaza Wadau wa Timu ya Taifa ya England alipotangaza uteuzi wake wa Kikosi chake cha Kwanza kabisa tangu athibitishwe kuwa Meneja wa kudumu kwa kuwaita Jermain Defoe, Jake Livermore na Luke Shaw pamoja na Wachezaji wengine Wanne wapya kabisa.

Kikosi kilichoitwa Leo ni Wachezaji 26 ambacho kitacheza na Mabingwa wa Dunia Germany na kisha Lithuania na wamo Wachezaji Wawili wa Southampton, James Ward-Prowse na Nathan Redmond, waliowahi kucheza chini ya Southgate alipokuwa Kocha Mkuu wa England U-21 lakini hawajahi kuchezea Kikosi cha Kwanza cha England.
Wengine wapya kabisa walioitwa Leo ni Michael Keane na Michail Antonio.
Related imageMarcus Rashford, Phil Jones na Ross Barkley wameitwa tena kuichezea Timu ya Taifa huku Straika wa Sunderland Jermaine Defoe, mwenye Miaka 34, ambae mara ya mwisho kuichezea England ni Novemba 2013, kuitwa tena kutokana na pengo la Mafowadi Majeruhi Wayne Rooney, Daniel Sturridge na Harry Kane.
Kwa mshangao wa wengi, Kiungo wa West Bromwich Albion, Jake Livermore, ameitwa baada ya kuichezea England mara moja tu Mwaka 2012 na 2015 kukumbwa na Skandali ya Matumizi ya Kokeni lakini akapata Msamaha baada ya Kifungo kifupi kwani wakati huo alifiwa na Mwanawe.
Pia, Luke Shaw, Fulbeki wa Kushoto wa Man United alieichezea Klabu yake mara 2 toka Novemba, amepata upenyo wa kuitwa tena kutoka na kuumia kwa Danny Rose wa Tottenham.

KIKOSI KAMILI:
MAKIPA:
Fraser Forster (Southampton), Joe Hart (Torino, Mkopo kutoka Man City), Tom Heaton (Burnley).

MABEKI:
Ryan Bertrand (Southampton), Gary Cahill (Chelsea), Nathaniel Clyne (Liverpool), Phil Jones (Man United), Michael Keane (Burnley), Luke Shaw (Man United), Chris Smalling (Man United), John Stones (Man City), Kyle Walker (Tottenham).

VIUNGO: Dele Alli (Tottenham), Michail Antonio (West Ham), Ross Barkley (Everton), Eric Dier (Tottenham), Adam Lallana (Liverpool), Jesse Lingard (Man United), Jake Livermore (West Brom), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Nathan Redmond (Southampton), Raheem Sterling (Man City), James Ward-Prowse (Southampton).

MAFOWADI:
Jermain Defoe (Sunderland), Marcus Rashford (Man United), Jamie Vardy (Leicester).