Friday, March 17, 2017

EPL: JUMAMOSI NA JUMAPILI KUPIGWA, MAN CITY v LIVERPOOL, SPURS vs SOUTHAMPTON, BORO vs MAN UNITED

TIMU ZOTE 20 za EPL, Ligi Kuu England, zipo dimbani Jumamosi na Jumapili na kisha Ligi hiyo kusimama hadi Aprili 1 kupisha Mechi za Kimataifa ambazo zipo Kalenda ya FIFA.

Mechi ya Awali kabisa Jumamosi ni huko The Hawthorns ambako West Bromwich Albion wataikaribisha Arsenal na kisha kufuata Mechi 5 za Saa 12 Jioni na miongoni mwake ni Stoke City kuwakaribisha Vinara Chelsea na Mabingwa Leicester City kuwa Wageni wa West Ham United huko London Stadium.
Mechi ya mwisho Jumamosi ni kati ya Bournemouth na Swansea City.
Jumapili zipo Mechi 3 ambako huko Riverside, Middlesbrough, baada ya Alhamisi kumtimua Swahiba mkubwa wa Jose Mourinho, Meneja Karanka, watamkaribisha Mourinho na Timu yake Man United.
Kisha itafuata Mechi ya huko Jijini London Uwanjani White Hart Lane kati ya Tottenham Hotspur na Southampton.

Mechi ya mwisho Siku hiyo ya Jumapili ni mtanange mkali huko Etihad kati ya Man City na Liverpool.


EPL – Ligi Kuu England
Ratiba:
Jumamosi Machi 18

1530 West Bromwich Albion v Arsenal
1800 Crystal Palace v Watford
1800 Everton v Hull City
1800 Stoke City v Chelsea
1800 Sunderland v Burnley
1800 West Ham United v Leicester City
2030 Bournemouth v Swansea City

Jumapili Machi 19

1500 Middlesbrough v Manchester United
1715 Tottenham Hotspur v Southampton 

1930 Manchester City v Liverpool