Sunday, March 5, 2017

EPL: LIVERPOOL YAITANDIKA ARSENAL BAO 3-1, WENGER APAGAWA!

LIVERPOOL jana wameitandika Arsenal 3-1 kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, iliyochezwa Anfield na kushika Nafasi ya 3 huku Arsenal wakishuka hadi Nafasi ya 5.
Kwenye Mechi hiyo, Dakika ya 9 Firmino aliipa Liverpool Bao kwa muvu iliyoanzia na Golkiki na kumfikia Coutinho aliepiga Kichwa kwa Lallana aliempa Mane ambae Krosi yake ya chini ilipenya na kumpita Coutinho ikimfikia Firmino aliepiga Shuti la chini ambalo na kumshinda Kipa Cech.

Dakika ya 39 ushirikiano wa upande wa kushoto wa Milner na Wijnaldum kumfikia Firmino ambae alimpasia Mane aliepiga Shuti la chini chini na kufunga.
Hadi Haftaimu Liverpool 2 Arsenal 0.
Arsenal walifunga Bao Dakika ya 56 kupitia Danny Welbeck alipopokea Pasi ya Alexis Sanchez alieingizwa Kipindi cha Pili kumbadili Coquelin.
Liverpool walijihakikishia ushindi Dakika ya 91 kwa Goli la Wijnaldum aliepokea pasi ya Origin a kufunga.

VIKOSI:
Liverpool (Mfumo 4-3-3):
Mignolet; Clyne, Matip, Klavan, Milner; Can, Wijnaldum, Lallana [Lucas, 92’], Mane [Alexander-Arnold, 93’], Firmino, Coutinho [Origi, 80’]
Akiba: Karius, Moreno, Lucas, Alexander, Lovren, Origi, Woodburn.

Arsenal (Mfumo 4-2-3-1):
Cech; Bellerin, Mustafi, Koscielny, Monreal; Coquelin [Sanchez, 45’], Xhaka; Oxlade-Chamberlain, Iwobi, Welbeck [Walcott, 74’], Giroud [Perez, 74’]
Akiba: Ospina, Gibbs, Gabriel, Ramsey, Alexis, Walcott, Lucas.