Thursday, March 16, 2017

EVERTON: ROMELU LUKAKU AGOMEA MKATABA MPYA, CHELSEA, MAN UNITED ZAMKODOLEA MACHO!

STRAIKA wa Everton Romelu Lukaku ameistua Everton kwa kutamka hatasaini Mkataba mpya wa Klabu hiyo ulioboreshwa kwa ajili yake.
Hivi karibuni, Wakala wa Lukaku, Mino Raiola,
alisisitiza Mbelgiji huyo hataihama Everton na tayari alishakubali kusaini Mkataba mpya ambao ungemfanya alipwe Pauni Laki 1 kwa Wiki na yeye kuwa ndie Mchezaji mwenye Mshahara mkubwa katika Historia ya Everton.
Licha ya Raiola kutoa uhakika huo, Meneja wa Everton Ronald Koeman alionyesha wasiwasi wake alipotamka: "Siamini Mawakala!"
Na hilo limetimia baada ya Jana Lukaku, mwenye Miaka 23, kuongea na Kituo cha TV cha huko kwao Belgium na kukanusha Maswali yote Mawili kama kwamba yupo tayari kusaini Mkataba mpya wa Miaka 5 au kama yapo Mazungumzo kuhusu hilo.
Hivi sasa Lukaku amebakiza Miaka Miwili katika Mkataba wake wa sasa lakini amepanda chati mno hasa baada ya Msimu huu kupiga Bao 19 kwenye Ligi Kuu England.
Mwanzoni mwa Msimu huu, Chelsea, ambako ndiko alikotoka na kwenda Everton kwa Mkopo na kisha kuhama moja kwa moja, walitaka kumnunua tena.
Pia zipo ripoti kuwa Man United wanamtaka licha ya kuripotiwa kumlenga Antoine Griezmann wa Atl├ętico Madrid na pia kutaka kumbakisha Mkongwe Zlatan Ibrahimovic kwa Msimu mmoja zaidi.
Ingawa zipo kila dalili sababu za Kifedha zitashindwa kuwafanya Everton kumng'ang'ania Lukaku baada ya Msimu huu kwisha, Klabu hiyo inaamini hamna kutoelewana kati yao na kambi ya Lukaku.