Saturday, March 18, 2017

FULL TIME - ASFC: KAGERA SUGAR 1 vs 2 MBAO FC

Kikosi cha Timu ya Mbao Fc cha Jijini Mwanza Kilichoifunga Timu ya Kagera Sugar bao 2-1 jioni hii kwenye Mtanange wa Azam Sports Federation Cup. Bao za mbao Fc zilifungwa kipindi cha kwanza, Bao la kwanza dakika ya 42 kipindi cha kwanza Salmin Hoza na kipindi cha pili dakika ya 84 Dickson Ambundo. Bao la pekee la Kagera Sugar lilifungwa dakika ya 90. Ushindi huu umewafanya Mbao Fc watangulie Nusu Fainali ya Kombe hili la Shirikisho, Kesho Mjini Arusha kutapigwa mchezo mmoja kati ya Madini Fc na Simba ya Jijini Dar es salaam. Mshindi ataungana na Mbao Fc. Picha zote na Faustine Ruta, Bukoba.
Mbaraka Yusuph akiendesha mpira ambaye anaongoza kwa ufungaji wa magoli Kagera Sugar. Kushoto ni Mchezaji wa Mbao FC Steve Mganya

Mchezaji wa Mbao FC Boniface Maganga  akigombea mpira na mchezaji wa Kagera Sugar Mohamed
Ame wa Kagera Sugar

Wachezaji wa Mbao Fc wakisgilia moja ya bao lao leo kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba leo.