Saturday, March 11, 2017

HATIMA YA REFA WA MECHI KATI YA PSG NA BARCA ALAUMIWA NA WENDA AKAFUNGIWA

Image result for deniz aytekinRefa Deniz Aytekin akiwapa Barca PenatiDeniz Aytekin, Refa ambae alisimamia wakati Barcelona ikiichakaza 6-1 Paris Saint-Germain kwenye Mechi ya Pili ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI, huenda akatupwa nje ya Marefa wa Mashindano hayo kutokana na uchezeshaji wake unaodaiwa kuinufaisha mno Barcelona na kusonga Robo Fainali baada ya kupiga Mechi ya Kwanza 4-0.Pierluigi Collina, Mkuu wa Marefa wa UEFA, ndie anaepanga Refa yupi anachezesha Mechi zipi za UCL na UEFA EUROPA LIGI.
Inasemekana Collina sasa anapitia Ripoti ya Uchezeshaji wa Aytekin, Refa kutoka Germany mwenye Asili ya Uturuki ambae ana Umri wa Miaka 38.
UEFA bado haijathibitisha uamuzi wa Collina lakini habari za chini chini zinadai Refa huyo ana uwezekano mdogo kusimamia tena Mechi za Ulaya Msimu huu.
UEFA imedokeza kuwa ili kufuta na kupunguza makosa, Collina ana kawaida ya kuwaondoa Marefa ‘wabovu’ kwenye Mechi kubwa.

MATUKIO MAKUBWA YA REFA AYTEKIN:
-Penati aliyotoa Aytekin baada Luis Suarez kujiangusha haikustahili.
Penati hii ilizaa Bao la 5 la Barca.
-Penati ya Neymar kuanguka wakati Beki wa PSG Thomas Meunier nayo haikustahili. Penati hii ilizaa Bao la 3 la Barca.
-Mascherano wa Barca alimchezea Faulo Di Maria ilistahili Penati lakini haikutolewa.