Monday, March 20, 2017

KOMBE LA DUNIA 2018 – MAREKANI KUSINI: IJUMAA VINARA URUGUAY vs BRAZIL

Mechi za Nchi za Kanda ya Marekani ya Kusini chini ya Mwamvuli wa Shirikisho lao CONMEBOL kusaka Nchi 4 zitakazotinga moja kwa moja huko Russia Mwaka 2018 kwenye Fainali za Kombe la Dunia, zitaendelea Alhamisi Wiki hii.
Baada ya Mechi 12 kwa kila Timu, Brazil ndio wanaongoza wakiwa na Pointi 27 wakifuata Uruguay wenye 23, Ecuador wana 20, Chile 20 na Argentina 19.
Kwenye Mechi za Wiki hii, mpambano mkali uko huko Montevideo wakati Wenyeji Uruguay wakikwaana na Brazil.
Mechi nyingine kali ni ile itakayochezwa Buenos Aires kati ya Argentina na Chile.
Nyingine ni kati ya Colombia na Bolivia, Paraguay na Ecuador huku Venezuela wakiivaa Peru. 

Raundi nyingine ya Kanda hii itaanza kuchezwa Jumanne Machi 28 na Siku inayofuatia ambapo Vinara Brazil watakuwa kwao kuivaa Paraguay.

MSIMAMO:
CONMEBOL
Kombe la Dunia – Russia 2018
Mechi za Makundi
Alhamsi Machi 23, 2017
23:30 Colombia v Bolivia

Ijumaa Machi 24, 2017
02:00 Paraguay v Ecuador
02:00 Uruguay v Brazil
02:30 Venezuela v Peru
02:30 Argentina v Chile

Jumanne Machi 28, 2017
23:30 Bolivia v Argentina

Jumatano Machi 29, 2017
00:01 Ecuador v Colombia
01:00 Chile v Venezuela
03:45 Brazil v Paraguay
05:15 Peru v Uruguay