Sunday, March 5, 2017

KUPIGWA 3 NA LIVERPOOL, SANCHEZ BENCHI, WENGER ALAUMIWA KWA KIPIGO

Arsenal boss Arsene Wenger shows his displeasure after watching his side go 2-0 down in the first-half at AnfieldWengerGeorginio Wijnaldum fires home on the break to complete a 3-1 win for Liverpool in the final minute against ArsenalLICHA kulaumiwa mno kwa uamuzi wake wa kumpiga Benchi Staa wake Alexis Sanchez kwenye Mechi Arsenal waliyotwangwa 3-1 hapo Jana huko Anfield na Liverpool, Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ametetea uamuzi wake huo wa kutomuanzisha Sanchez.
Wakiwa 2-0 nyuma, Wenger alimuingiza Sanchez wakati wa Haftaimu na yeye ndio alietoa Pasi ambayo Danny Welbeck aliifungia Arsenal Bao lao Moja.
Msimu huu, Sanchez ameshiriki katika Bao 26 za Arsenal akifunga 17 na kusaidia 9.
Baada ya Mechi hiyo, Wenger alieleza: “Kila Mtu ana maoni yake. Mie nina nguvu na ujuzi wa kujua nini matokeo ya uamuzi ule!”
Jurgen Klopp lets out a roar and clenches his fist in celebration after Mane's goal put his Liverpool side 2-0 upKwenye Mechi ya Jana, badala ya kumtumia Sanchez, Wenger aliamua kuwaweka pamoja Welbeck na Oliver Giroud. The Senegalese international celebrates with Philippe Coutinho after scoring his 12th goal of the seasonAmeeleza: “Nilitaka kuwaanzisha Wachezaji ambao ni wazuri kwa Mipira ya juu na kisha kumuingiza Sanchez Kipindi cha Pili.” 

MARTIN KEOWN, Beki wa zamani wa Arsenal, akiongea na BBC alisema: “Kumpiga Benchi Sanchez kulishtua! Sielewi ni kwanini. Yeye ndie Mchezaji wao Bora! Sikumbuki katika Miaka 20 ya Wenger wakicheza Soka bovu lilikosa ari na moyo kama lile!” Wijnaldum celebrates in front of the Kop as Liverpool climbed up to third in the Premier League tableWenger amekiri uamuzi wa kumpiga Benchi Sanchez haukuwa rahisi.
Kipigo cha Liverpool ni cha 3 kwa Arsenal katika Mechi zao 4 za Ligi zilizopita na kuwatupa Nafasi ya 5 kwenye Ligi wakiwa Pointi 2 nyuma ya Timu ya 4 Man City ambao wana Mechi 1 mkononi.