Monday, March 13, 2017

LA LIGA: BARCELONA YAFUNGWA BAO 2-1 NA DEPORTIVO LA CORUNA, YATOA MWANYA KWA REAL!

Mabingwa Watetezi wa La Liga Barcelona Leo wametandikwa Bao 2-1 na Deportivo La Coruna huko Estadio Municipal de Riazor, katika Mechi ya La Liga ambayo imetoa mwanya kwa Real Madrid kushika uongozi ikiwa Usiku huu wataifunga Real Betis Uwanjani Santiago Bernabeu.
Deportivo La Coruna walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 40 la Joselu ambalo lilidumu hadi Mapumziko.
Luis Suarez akaisawazishia Barca Dakika ya 46 lakini Bergantiños García akaipa ushindi Deportivo La Coruna kwa Bao la Dakika ya 74.
Barca bado wamebaki kileleni mwa La Liga wakiwa na Pointi 60 kwa Mechi 27 wakifuata Real wenye Pointi 59 kwa Mechi 25.
Deportivo La Coruna wao wapo nafasi ya 15 wakiwa na Pointi 27 kwa Mechi 27.


LA LIGARATIBA/MATOKEO
Ijumaa Machi 10

RCD Espanyol 4 Las Palmas 3

Jumamosi Machi 11
Granada CF 0 Atletico de Madrid 1
Valencia 1 Sporting Gijon 1
Sevilla 1 CD LAeganes 1
Malaga 1 Alaves 2

Jumapili Machi 12

Real Sociedad 0 Athletic de Bilbao 2
Deportivo La Coruna 2 FC Barcelona 1
Celta de Vigo v Villarreal CF
Real Madrid CF v Real Betis

Jumatatu Machi 13
Osasuna v SD Eibar