Sunday, March 19, 2017

FULL TIME EPL: MIDDLESBROUGH 1 vs 3 MANCHESTER UNITED, VICTOR VALDES AAIBIKA DAKIKA ZA LALA SALAMA, MAN U WAIBUKA KIDEDEA NA KUPANDA NAFASI YA 5!

Zikiwa zimebaki dakika za majeruhi Kipa wa zamani wa Man
United alipigiwa mpira na katika kutaka kuokoa kwa kuurudisha mpira huo mbele aliteleza chini na mchezaji nambari 25 Valencia, aliupata na kuukokota nyavuni mwa lango lao Boro na kuifanya Man United iibuke na ushindi wa bao 3-1. Middlesbrough, maarufu kama Boro, wamepigwa Bao 3-1 na Manchester United na kudidimizwa mkiani huku Man united wakipanda hadi Nafasi ya 5 na kuwashusha Arsenal kushika Nafasi ya 6.
Hii ni Mechi ya kwanza kwa Boro tangu wamtimua Meneja wao Aitor Karanka hapo juzi ambae alikuwa Swahiba mkubwa wa Jose Mourinho, Meneja wa Man United.

Middlesbrough 1-3 Man United: Mourinho's side move fifthMan United walianza Mechi hii wakiwa na Kikosi kilichobadilika Wachezaji 7 toka kile kilichoifunga FC Rostov 1-0 Juzi Alhamisi kwa Kipa David De Gea kurejea Golini huku Zlatan Ibrahimovic na Ander Herrera wakikosekana kwa kuwa Vifungoni na Paul Pogba kuwa Majeruhi.
Man United walipata Bao Dakika ya 30 kufuatia Krosi ya Ashley Young kutoka Kushoto kuunganishwa kwa Kichwa na Marouane Fellaini na kumpita Kipa wa zamani wa Man United Victor Valdes.
Hadi Haftaimu Middlesbrough 0 Man United 1.

Bao la pili la Man United lilifungwa kipindi cha pili dakika ya 62 na Jesse Lingard baada ya kutembea na mpira ndani ya 18 na kuachia shuti kali lililozama moja kwa moja nyavuni na Man United kujipatia bao la 2.1-0 Wachezaji wa Man United wakipongezana na Maruane Fellaini kipindi cha kwanza mara baada ya kuwapachikia bao la kuongoza katika kipindi hicho cha kwanza.Marouane Fellaini dakika ya (30') anaipachikia bao safi kwa kichwa baada ya kupata klosi safi kutoka kwa Ashley Young. Ikiwa ni baada ya patashika kubwa huku Marcus Rashford akijaribu kumfunga kipa wa zamani wa Man United Victor Valdes mara mbili akiokoa kipa huyo.
KWENYE REKODI:
Huu ni ushindi wa 600 wa Man United kwenye EPL na ni Rekodi {Sare 204 Kufungwa 147}
Wanaofuata ni Arsenal Walioshinda 517, Chelsea 508 na Liverpool 472

Rashford kaanzaMiddlesbrough v Manchester United, EPL LIVE score