Sunday, March 19, 2017

FULL TIME EPL: MANCHESTER CITY 1 vs 1 LIVERPOOL, SERGIO AGUERO AIKOA CITY KWAO NA KUUMALIZA KWA SARE!

Manchester City na Liverpool zimetoka Sare 1-1 huko Etihad kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
Matokeo haya yamezibakisha Timu zote hizo mbili Nafasi zao zile zile kwenye EPL City wakiwa Nafasi ya 3 na Liverpool Nafasi ya 4.

Liverpool ndio waliotangulia kufunga Bao kwa Penati ya James Milner ya Dakika ya 51 iliyotolewa baada ya Gael Clichy kumchezea Rafu Firmino.
City walisawazisha Dakika ya 69 Mfungaji akiwa Sergio Aguero aliemalizia Pasi ya chini kutoka kwa Kevin De Bruyne.
EPL sasa inasimama kupisha Mechi za Kimataifa zilizo kwenye Kalenda ya FIFA na itarejea tena Aprili 1.
Kipindi cha pili Sergio Ag├╝ero dakika ya (69') aliwasawazishia Bao Manchester City na kufanya matokeo kuwa 1-1 na Mashabiki wao Kushangilia kwenye Uwanja huo wa Etihad. Kipindi cha pili dakika ya 51 James Milner aliwapachikia bao Liverpool kwa mkwaju wa penati.