Wednesday, March 29, 2017

MAN UNITED KAZI WANAYO MWEZI APRILI, MECHI 9 NDANI YA SIKU 30.

Related imagePogbaBAADA ya kukaa pembeni kwa Wiki Mbili kupisha Mechi za Kimataifa, Manchester United wanarudi kilingeni Jumamosi Aprili 1 kwa kucheza Nyumbani Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, dhidi ya West Bromwich Albion Uwanjani Old Trafford.
Mechi hiyo ni mwanzo wa mfululizo wa Mechi 9 ambazo watazicheza Mwezi Aprili na 7 kati ya hizo ni za EPL wakati 2 ni za UEFA EUROPA LIGI za Robo Fainali wakipambana na Klabu ya Belgium Anderlecht.
Hivi sasa Man United wapo Nafasi ya 5 kwenye Ligi wakiwa na Pointi 52 kwa Mechi 27 wakiwa nyuma ya Timu ya 4 Liverpool kwa Pointi 2 lakini Liverpool wamecheza Mechi 2 zaidi yao wakati Timu ya 3, Man City, wakiwa mbele yao kwa Pointi 5 lakini nao wamecheza Mechi 1 zaidi yao.
Timu ya Pili ni Tottenham wenye Pointi 59 kwa Mechi 28 na Vinara ni Chelsea wenye Pointi 69 kwa Mechi 28.
Mbali ya kuwania Nafasi ya 4 Bora kwenye EPL ili wacheze UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao, Man United wanaweza kutinga Mashindano hayo ikiwa watatwaa UEFA EUROPA LIGI na hivyo kikwazo cha kwanza kwao ni kuing’oa Anderlecht.
Lakini Mechi hizi mfululizo kwao si rafiki wao na hasa wakiwa na Majeruhi na Vifungo kwa Wachezaji wao.

http://e2.365dm.com/17/02/16-9/20/skysports-zlatan-ibrahimovic-manchester-united-efl-cup-final-trophy_3898689.jpg?20170226190512Mfungaji wao Bora Zlatan Ibrahimovic na Kiungo Ander Herrera wapo Vifungoni na wote wataikosa Mechi na West Bromwich Albion wakimalizia Vifungo vyao vya Mechi 3 kwa Ibrahimovic na 2 kwa Herrera.
Lakini pia Mechi hiyo itawakosa Majeruhi Chris Smalling, Phil Jones, Marouane Fellaini na pengine Paul Pogba.

http://video.skysports.com/NjNXAzOTE65pS9yjIY6TJakc-p4u40BJ/promo309288088MAN UNITED – RATIBA MWEZI APRILI 2017:
01 APR: Man United v West Bromwich Albion, EPL, Saa 1700
04 APR: Man United v Everton, EPL, 2200
09 APR: Sunderland v Man United, EPL, 1530
13 APR: Anderlecht v Man United, Europa Ligi Robo Fainali, 2205
16 APR: Man United v Chelsea, EPL, 1800
20 APR: Man United v Anderlecht, Europa Ligi Robo Fainali, 2205
23 APR: Burnley v Man United, EPL, 1615
27 APR: Man City v Man United, EPL, 2200
30 APR: Man United v Swansea City, EPL, 1400