Wednesday, March 22, 2017

MAN UNITED YAMRUHUSU SCHWEINSTEIGER KUJIUNGA CHICAGO FIRE - USA

KIUNGO kutoka Germany Bastian Schweinsteiger ameruhusiwa na Klabu yake Manchester United kujiunga na Chicago Fire inayocheza Ligi MLS huko USA.
Schweinsteiger alijiunga na Man United iliyokuwa chini ya Louis van Gaal kutoka Bayern Munich Julai 2015 kwa Dau la Pauni Milioni 14.4 lakini tangu aingie Jose Mourinho madarakani mwanzoni mwa Msimu huu Mchezaji huyo amekuwa hayupo Kikosi cha Kwanza.
Dili ya Schweini kuhamia Chicago Fire ilikamilika Jana na Uhamisho wake utakuwa rasmi baada ya kukamilisha upimwaji Afya yake na kupata Visa.
Kwa mujibu wa Gazeti Chicago Tribune la huko Marekani, Schweinsteiger, mwenye Miaka 32, amesaini Mkataba wa Mwaka Mmoja na Chicago Fire wenye kipengele cha Nyongeza ya Mwaka Mmoja.

http://www.manutd.com/~/media/AD6C95AE4A6542FDB80473ADEAA43787.ashxSchweinsteiger, ambae aliiongoza Germany kutwaa Kombe la Dunia Mwaka 2014, ilikuwa ahamie Chicago Fire tangu Januari lakini akaamua kubaki Man United.
Hata hivyo, Kiungo huyo amekuwa hana thamani kwa Mourinho na alicheza Mechi yake ya kwanza Msimu huu ya EFL CUP dhidi ya West Ham hapo Novemba 30.
Baada ya hapo alicheza Mechi 3 zaidi na ya mwisho ni ile dhidi ya Saint-Etienne kwenye UEFA EUROPA LIGI hapo Februari 22.