Tuesday, March 28, 2017

MATUSI YAMFUNGISHA LIONEL MESSI KUIKOSA BOLIVIA USIKU HUU

KEPTENI wa Argentina Lionel Messi huenda Leo akaikosa Mechi ya Nchi yake na Bolivia ambayo ni ya Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini kusaka kufuzu Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.
Juzi Argentina iliifunga Chile 1-0 kwa Penati ya Messi lakini imedaiwa kwenye Mechi hiyo Staa huyo alimshambulia Mshika Kibendera Marcelo Van Gasse kwa Matusi makali katika Kipindi cha Pili cha Mechi hiyo.
Pia inasemekana mwishoni mwa Mechi hiyo Messi alikataa kumpa mkono Refa huyo Msaidizi.
Hata hivyo, tukio hilo halikuwekwa kwenye Ripotri ya Awali ya Refa wa Mechi lakini Jana likaongezwa na kupelekwa CONMEBOL ambalo ndio Shirikisho la Soka la Nchi za Marekani ya Kusini.
Sasa kinangojewa uamuzi wa Kamati ya Nidhamu ya CONMEBOL ambayo inaweza kutoa Adhabu mara moja na hivyo Messi kuikosa Mechi ya Argentina na Bolivia huko La Paz hii Leo ama kuamuru Kifungo kiwe baada ya Mechi hii.

Ikiwa atafungiwa kwa Mechi ya Leo, Argentina wakikata Rufaa Messi anaweza Leo kucheza na Kifungo chake kutumika baada ya Rufaa kuamuliwa ikiwa atashindwa na Mechi itakayohusika ni ya Mwezi Agosti na Uruguay.

Hivi sasa Argentina wapo Nafasi ya 3 kwenye Kundi hili la Kombe la Dunia 2018 wakiwa nyuma ya Vinara Brazil na Uruguay.


JE WAJUA?
-CONMEBOL
itatoa Nchi 4 kutinga Fainali za Kombe la Dunia huko Russia Mwaka 2018.
-Nchi hizo zinaweza kuwa 5 ikiwa Timu itakayomaliza Nafasi ya 5 kwenye Kundi lao itashinda Mechi ya Mchujo dhidi ya Timu nyingine toka Bara jingine ambayo itakuwa ni moja toka Kanda ya Oceania yenye Nchi za Visiwani ambazo ni New Zealand, New Caledonia, Fiji, Papua New Guinea, Solomon Islands na Tahiti. 


CONMEBOL
Kombe la Dunia – Russia 2018
Mechi za Makundi
Ratiba:
Jumanne Machi 28, 2017

2330 Bolivia v Argentina

Jumatano Machi 29, 2017
0001 Ecuador v Colombia
0100 Chile v Venezuela
0345 Brazil v Paraguay
0515 Peru v Uruguay