Thursday, March 16, 2017

MIDDLESBROUGH YAMTIMUA KARANKA

Aitor Karanka ametimuliwa Umeneja na Middlesbrough ambayo ni maarufu kama Boro.
Karanka, Raia wa Spain mwenye Miaka 43, ameondolewa Asubuhi hii akiiacha Timu hiyo aliyodumu nayo kwa Miaka Mitatu na Nusu ikiwa Nafasi ya 19 kati ya Timu 20 za EPL, Ligi Kuu England.

Boro hawajashinda katika Mechi 10 za Ligi, mara ya mwisho ikiwa Desemba 17, huku wakifunga Bao 3 tu katika kipindi hicho. Aliekuwa Msaidizi wa Meneja, Steve Agnew, ndie atakaimu nafasi ya Karanka.
Kutimuliwa kwa Karanka, ambae ni swahiba mkubwa wa Meneja wa Man United, Jose Mourinho, Timu ambayo Boro wataivaa katika Mechi ya Ligi inayofuata, kulitangazwa kwenye Tovuti ya Klabu hiyo Asubuhi hii.

Karanka na Mourinho walikuwa wote huko Real Madrid baada ya Mourinho kumteua kuwa Msaidizi wake Juni 2010.
Licha ya kusuasua, Karanka aliamini atarekebisha mambo kwenye Mechi zao 11 za Ligi walizobakisha na hasa alipata imani hiyo baada ya kucheza vizuri Mechi yao ya mwisho walipopigwa 2-0 na Man City kwenye Robo Fainali ya FA CUP Jumamosi iliyopita.