Tuesday, March 28, 2017

PODOLSKI AIAGA RASMI GERMANY KWA KUIBAMIZA ENGLAND BAO 1-0.

LUKAS PODOLSKI amestaafu rasmi kuichezea Timu ya Taifa ya Germany Jana kwa kuiongoza kama Nahodha na pia kufunga Bao pekee na la ushindi walipowafunga England 1-0 huko Signal Iduna Park Jijini Dortmund Nchini Germany.
Hicho kilikuwa kipigo cha kwanza kwa Meneja wa England Gareth Southgate katika Mechi zake 4 tangu ashike wadhifa Mwaka Jana kutoka kwa Sam Allardyce.
Bao hilo la Podolski lilifungwa Dakika ya 69 kwa kigongo toka nje ya Boksi na kumshinda Kipa wa England Joe Hart.

England walikosa Bao baada ya Adam Lallana kupigacPosti na Shuti la Dele Alli kuokolewa na Kipa wa Germany Marc-Andre ter Stegen kwenye Kipindi cha Kwanza ambacho England walikuwa juu.

VIKOSI:
Germany (4-2-3-1)
Ter Stegen; Kimmich, Rudiger, Hummels, Hector; Weigl (Can 66), Kroos; Sane, Podolski (Rudy 84), Brandt (Schurrle 59), Werner (Muller 77)

England (3-4-2-1): Hart; Keane, Smalling (Stones 84), Cahill; Walker, Dier, Livermore (Ward-Prowse 83), Bertrand (Shaw 83), Lallana (Redmond 66), Alli (Lingard 71), Vardy (Rashford 70)
REFA: Damir Skomina (Slovenia)