Wednesday, March 22, 2017

SIR ALEX FERGUSON KUREJEA TENA OLD TRAFFORD, ASEMA UNITED WATAKIWA KUBEBA EUROPA LEAGUE!

Sir Alex Ferguson atarudi tena Old Trafford kwenye Benchi wakati wa Mechi ya Kumtukuza Kiungo wa Manchester United Michael Carrick kwa Utumishi Ulitukuka wa muda mrefu Klabuni hapo.
Ferguson, aliestaafu Umeneja Mwaka 2013 baada ya kuitumikia Man United kwa Miaka 27, ataongoza moja ya Timu katika Mechi hiyo Maalum.
Timu atakayoongoza Sir Alex Ferguson itaitwa Manchester United 2008 XI na itaundwa na Wachezaji waliotwaa Ubingwa wa England na UEFA CHAMPIONS LIGI Mwaka 2008 wakiwa chini yake.
Timu hiyo itacheza na Timu itakayoitwa Michael Carrick All-Star XI ikiongozwa na aliewahi kuwa mmoja wa Mameneja wa Michael Carrick, Harry Redknapp.

Carrick, mwenye Miaka 35 na ambae amedumu Man United kwa Miaka 11 hadi sasa, ameelezea kurejea kwa Sir Alex Ferguson: “Ni heshima kubwa kurejea kwake na kuwa sehemu ya hiyo Gemu. Yeye pengine ndio sababu pekee nilijiunga na Man United, sina uwezo kumshukuru inavyostahili!”

Miongoni mwa Majina makubwa ya Wachezaji Soka watakaoshiriki Mechi hiyo maalum ni Edwin van der Sar, Gary Neville, Rio Ferdinand, Paul Scholes na Ryan Giggs wakiichezea Man United na upande wa Michael Carrick All-Star XI watakuwemo Steven Gerrard, Frank Lampard na Michael Owen.
Ferguson was manager at United for 27 years between 1986 and 2013Ferguson amekuwa Meneja wa United kwa miaka 27 kwenye miaka ya 1986 na 2013