Wednesday, March 22, 2017

TOTAL CAF KOMBE LA SHIRIKISHO: YANGA YAPANGWA NA TIMU YA ALGERIA

MABINGWA WA TANZANIA BARA, Yanga, ambao Juzi walitupwa nje ya TOTAL CAF CHAMPIONS LIGI na kuangukia TOTAL CAF Kombe la Shirikisho, Leo wamepangwa kucheza Raundi ya Mchujo na Klabu ya Algeria MC Alger.
Mc Alger, kirefu ni Mouloudia Club d'Alger, ni Klabu ambayo Makao Makuu yake ni Mji Mkuu wa Algeria, Algiers.
Washindi 16 wa Raundi hiyo watacheza Hatua ya Makundi.
Droo ya Raundi ya Mchujo ya TOTAL CAF Kombe la Shirikisho imefanyika muda mchache uliopita huko Makao Makuu ya CAF Jijini Cairo Nchini Egypt.
Droo hii imekutanisha Timu 16 zilizoshinda Raundi ya Kwanza ya Mashindano haya na kupambanishwa na Timu 16 zilizotupwa nje ya Raundi ya Kwanza ya CAF CHAMPIONZ LIGI na mojawapo ni hii Yanga yetu.

DROO KAMILI:
CAF KOMBE LA SHIRIKISHO
Raundi ya Mchujo

Young Africans v MC Alger

TP Mazembe v JS Kabylie
AC LĂ©opards v Mbabane Swallows
FUS Rabat v MAS Fez
Enugu Rangers v ZESCO United
CF Mounana v ASEC Mimosas
Rail Club du Kadiogo v CS Sfaxien
Bidvest Wits v Smouha
CNaPS Sport v Recreativo do Libolo
KCCA v Al-Masry
Gambia Ports Authority v Al-Hilal Al-Ubayyid
AS Port-Louis 2000 v Club Africain
Rivers United v Rayon Sports
Barrack Young Controllers v SuperSport United
AS Tanda v Platinum Stars
Horoya v IR Tanger 


Mechi kuchezwa Aprili 7-9 na Marudiano ni Aprili 14-16.
-Washindi 16 kusonga Hatua ya Makundi