Friday, March 17, 2017

UEFA CHAMPIONS LIGI – DROO ROBO FAINALI: MABINGWA REAL MADRID vs BAYERN, JUVENTUS vs BARCELONA

DROO ya kupanga Mechi za Robo Fainali za UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL, imefanyika Mchana huu huko Nyon, Uswisi kwenye Makao Makuu ya UEFA na Mabingwa Watetezi Real Madrid kupangwa na Bayern Munich.
Mabingwa wa England Leicester City wao wamepangwa kucheza na Atletico Madrid wakati Barcelona wakicheza na Juventus na Borussia Dortmund kuivaa AS Monaco.

ROBO FAINALI – DROO KAMILI:
-Atletico Madrid v Leicester City
-Borussia Dortmund v AS Monaco
-Bayern Munich v Real Madrid
-Juventus v Barcelona

Mechi za Robo Fainali zitachezwa Aprili 11 na 12 na Marudiano ni Aprili 18 na 19.
TAREHE MUHIMU:

MECHI ZA MTOANO:
11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza
18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili
02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza
09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili
03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)