Thursday, March 16, 2017

UEFA EUROPA LEAGUE: ALHAMISI MAN UNITED vs FC ROSTOV, MBWANA SAMATTA NAE KWENYE PATASHIKA KATI YA KRC GENK vs KAA GENT

Mechi za Pili za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA EUROPA LIGI zitachezwa Alhamisi na mvuto mkubwa ni huko Old Trafford Jijini Manchester, England na kule Fenix Stadion Jijini Genk, Belgium.
Huko Old Trafford, Manchester United, baada ya kupata Sare 1-1 huko Rostyov Wiki iliyopita kwenye Uwanja mbovu ambao sasa umefungiwa, watarudiana tena na FC Rostov wakihitaji Sare ya 0-0 au ushindi ili kutinga Robo Fainali.
Meneja wa Man United, Jose Mourinho, amesema licha ya kulazimika kucheza mfululizo na hasa Jumatatu Usiku walipotolewa 1-0 kwenye FA CUP na Chelsea Kikosi chake ki tayari ingawa kitawakosa Majeruhi Kepteni wao Wayne Rooney na Anthony Martial.

Lakini habari njema kwao ni kurejea Kikosini kwa Mfungaji wao mkubwa Zlatan Ibrahimovic alieikosa Mechi ya Chelsea kutokana na kuwa Kifungoni Mechi 3.
Kifungo hicho ni kwa Mechi za England tu na hakihusiana na Mechi za Ulaya,
Wiki iliyopita, wakiwa Ugenini kwa Mahasimu wao wa Nchini kwao Belgium, KRC Genk iliichapa KAA Gent 5-2 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi hii huku Shujaa wa Tanzania, Mbwana Samatta, akipiga Bao 2.
Safari hii, Mechi ya Marudianio ipo Nyumbani kwa KRC Genk, Fenix Stadion Jijini Genk, ambao wanatarajia matokeo mema ili kutinga Robo Fainali.

Droo za Robo Fainali zitafanyika Ijumaa.
UEFA EUROPA LEAGUE
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
Mechi za Kwanza [Marudiano Machi 16]

Matokeo:
EUROPA LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16 – Mechi za Pili
Ahamisi Machi 16 

Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza
2100 Besiktas v Olympiakos (1-1)
2100 FK Krasnodar v Celta Vigo (1-2)
2100 KRC Genk v KAA Gent (5-2)
2305 Ajax v FC Copenhagen (1-2)
2305 Borussia Mönchengladbach v FC Schalke 04 (1-1)
2305 Manchester United v FC Rostov (1-1)
2305 Roma v Lyon (2-4)
2305 RSC Anderlecht v Apoel Nicosia (1-0)

UEFA EUROPA LIGI
Tarehe Muhimu:

13/04/17: Robo Fainali, Mechi za Kwanza
20/04/17: Robo Fainali, Mechi za Pili
04/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza
11/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili
FAINALI
24 Mei 2017:
Friends Arena, Solna, Sweden