Friday, March 17, 2017

UEFA EUROPA LEAGUE – DROO YA ROBO FAINALI: ANDERLECHT vs MANCHESTER UNITED. CELTA VIGO vs KRC GENK

DROO ya Mechi za Robo Fainali ya UEFA EUROPA LIGI imefanyika Leo huko Nyon, Uswisi kwenye Makao Makuu ya UEFA na Manchester United kupangwa kucheza na Anderlecht ya Belgium.
Timu anayochezea Staa mkubwa wa Tanzania, Mbwana Samatta, KRC Genk ya Belgium, wao watawavaa Celta Vigo ya Spain.
Mechi nyingine ni kati ya Ajax na Schalke wakati Lyon ya France wakicheza na Besiktas ya Uturuki.

Robo Fainali – Droo kamili:
-Anderlecht v Manchester United
-Celta Vigo v KRC Genk
-Ajax v Schalke
-Lyon v Besiktas


Mechi za Robo Fainali zitachezwa Aprili 13 na Marudio ni Aprili 20.
UEFA EUROPA LIGI
Tarehe Muhimu:

13/04/17: Robo Fainali, Mechi za Kwanza
20/04/17: Robo Fainali, Mechi za Pili
04/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza
11/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili

FAINALI
24 Mei 2017: Friends Arena, Solna, Sweden