Sunday, March 5, 2017

VPL: YANGA YABANWA NA MTIBWA, WATOKA SARE YA 0-0

MABINGWA Watetezi wa VPL, Ligi Kuu England, Yanga, Leo wameshindwa kuing’oa Simba toka kileleni mwa Ligi baada ya kutoka Sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar huko Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro.
Yanga wangeweza kushinda Mechi hii baada ya kupewa Penati ya Dakika ya 34 lakini Mchezaji wao Simon Msuva akashindwa kuifunga Penati hiyo.
Kwa Matoke ohayo Yanga wanabaki Nafasi ya Pili nyuma ya Simba ambao wako Pointi 2 mbele yao baada ya Jana kutoka Sare 2-2 na Mbeya City.
Katika Mechi nyingine iliyochezwa Leo, African Lyon iliitungua Mwadui FC 1-0 kwa Bao la Fred Lewis.
VPL itaendelea Jumatatu kwa Mechi 1 kati ya Ndanda FC na Ruvu Shooting huko Nangwanda, Mtwara na Jumamosi ijayo zipo Mechi nyingine 3 za Ligi huku mojawapo ikiwa huko Kaitaba, Bukoba kati ya Kagera Sugar na Simba.