Wednesday, March 8, 2017

WACHEZAJI 20 WA MAN UNITED WAPAA URUSI KUIVAA FC ROSTOV, MASHABIKI WAO WAONYWA KUTOVAA JEZI ZA TIMU KUKWEPA VURUGU!

MASHABIKI wa Manchester United wameonywa kutovaa Jezi za Klabu hiyo wakiwa huko Russia.
Man United itaivaa FC Rostov Alhamisi Usiku huko Mjini Rostov Nchini Russia kwenye Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA EUROPA LIGI.
Ili kukwepa vurugu kama zile zilizotokea huko France Mwezi Juni wakati wa Fainali za EURO 2016 wakati Mashabiki wa Russia walipowashambulia wale wa England, Mashabiki wa Man United wameshauriwa kutovaa Jezi za Klabu hiyo wakiwa matembezini Mjini Rostov.

Mkuu wa Kitengo cha Tiketi na Uanachama cha Man United, Sam Kelleher, amewaandikia Mashabiki wote wanaosafiri kwenda Rostov kuwapa ushauri wa kujilinda wakiwa huko Russia.

Mbali ya kushauriwa kutovaa Jezi za Man United wakiwa matembezini Mjini Rostov, pia wametakiwa kutotembea mmoja mmoja bali wawe kwenye vikundi.

WAKATI HUO HUO, Meneja Jose Mourinho ameteua Wachezaki 20 walioruka Jioni hii kwenda huko Urusi na Kepteni Wayne Rooney hayumo Kikosini.

Pia Luke Shaw na Bastian Schweinsteiger hawamo kwenye Kikosi hicho pamoja na Eric Bailly ambae yuko Kifungoni Mechi 1 baada ya kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu katika Mechi iliyopita dhidi ya Saint-Etienne.

Habari njema kwa Man United ni kupona kwa Henrikh Mkhitaryan ambae aliumia kwenye Mechi na Saint-Etienne na kuzikosa Mechi 2 zilizopita zile za Fainali ya EFL CUP Man United ilipoifunga Southampton na kutwaa Kombe na ile Sare ya Juzi na Bournemouth.

KIKOSI KAMILI KILICHOSAFIRI:
De Gea, Romero, O'Hara; Valencia, Jones, Rojo, Smalling, Blind, Darmian, Young; Carrick, Herrera, Fellaini, Pogba, Mata, Lingard, Mkhitaryan; Martial, Rashford, Ibrahimovic.