Monday, April 3, 2017

ARSENE WENGER AJISOGEZA KWA MASHAKI WA ARSENO, LICHA KUMPINGA. SARE YAO NA CITY PIA WENGER ASEMA ''POA TU''

MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger amewasifu Mashabiki wa Timu hiyo kwa sapoti yao waliyoonyesha Uwanjani Emirates wakati walipotoka 2-2 na Manchester City licha ya baadhi yao kuaandamana kumpinga kumtaka aondoke Klabuni hapo.

Wenger hivi sasa yuko kwenye presha kubwa baada ya Arsenal kushinda Mechi 1 to kati ya 6 za EPL, Ligi Kuu England ambayo sasa wameporomoka hadi Nafasi ya 6.

Wenger ameeleza: “Licha yay ale yaliyotokea kwa Washabiki wetu, Leo wamekuwa imara zaidi katika wakati mgumu tulipokuwa nyuma 1-0 na kisha 2-1, wangeweza kutubadilika lakini walisimama kidete kutuvusha na kupata Sare!”
Jana Bao za Theo Walcott na Shkodran Mustafi zilifuta Bao za City za Leroy Sane na Sergio Aguero.
Wenger, ambae Mkataba wake na Arsenal unaisha mwishoni mwa Msimu huu, amepewa Ofa ya Mkataba Mpya wa Miaka Miwili na Arsenal na ameshasema uamuzi wa kubaki au kuondoka utatolewa hivi karibuni.
Jumatano Arsenal tena wapo kwao Emirates kuivaa West Ham na Jumatatu ijayo watacheza Ugenini na Crystal Palace zote zikiwa Mechi za EPL.