Sunday, April 30, 2017

ASFC: MBAO FC YAITUNGUA BAO 1-0 YANGA, SASA KUCHEZA FAINALI NA SIMBA

MBAO FC ya Mwanza Leo imefanikiwa kuwalaza waliokuwa Mabingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup - ASFC) Yanga Bao 1-0 huko CCM Kirumba Mwanza na kutinga Fainali ambayo watacheza na Simba.
Jumamosi Simba iliitoa Azam FC 1-0 katika Nusu Fainali nyingine.
Mshindi wa Kombe hili ndie ataiwakilisha Tanzania Bara katika Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho kwa Msimu ujao.
Bao pekee na la ushindi kwa Mbao FC lilipachikwa Dakika ya 27 na Vincent Andrew ‘Dante’ aliejifunga mwenyewe akiihami Krosi ya Pius Buswita.

VIKOSI:
MBAO FC:
Benedict Haule, David Mkwasa, Alex Ntiri, Boniface Maganga, Salmin Hoza, Yussuf Ndikumana, Jamal Mwambeleko, George Sangija, Everigustus Bernard [Robert Ndaki 73], Pius Buswita, Ibrahim Njohole

YANGA: Deogratius Munishi ‘Dida’, Hassan Kessy [Juma Abdul 67], Mwinyi Mngwali, Andrew Vicent ‘Dante’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Said Juma ‘Makapu’ [Geoffrey Mwashiuya 46], Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Obrey Chirwa [Emmanuel Martin 83], Amissi Tambwe, Haruna Niyonzima.