Wednesday, April 12, 2017

BAUZA ATIMULIWA ARGENTINA KWA MATOKEO MABAYA!

Argentina imemfukuza Menejabwao wa Timu ya Taifa Edgardo Bauza kufuatia matokeo mabovu yanayohatarisha.kufuzu kwao kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.
Bauza alisimamia Mechi 8 za Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini CONMEBOL za kusaka kwenda Fainali za huko Russia na wameshinda 3 tu kati ya hizo.
Hivi sasa Argentina wapo Nafasi ya 5 ya Nchi za Kanda ya Marekani ya Kusini nafasi ambayo itawanyima kufuzu moja kwa moja kwenda Russia.
Timu 4 za juu ndizo zinazofuzu moja kwa moja kwenda Fainali za Kombe la Dunia za huko Russia.
Timu inayomaliza Nafasi ya 5 hulazimika kucheza Mechi ya Mchujo na Nchi kutoka Kanda ya OCEANIA na Mshindi kutinga Russia.
Mbali ya kusuasua kwenye Mechi hizo za kwenda Russia, Argentina pia wapo kwenye pigo kubwa kutokana na Kifungo cha Mechi 3 cha Nahodha wao Lionel Messi kitakachomfanya acheze Mechi ya mwisho tu ya Kanda yao kwani wamebakiza Mechi 4 tu.

Bauza alishika Umeneja wa Argentina Agosti Mwaka Jana baada ya kujiuzulu kwa Gerardo "Tata" Martino alieng'oka baada ya Argentina kufungwa na Chile kwenye Fainali ya Copa America Centenario.
Muargentina ambae ni Kocha wa Sevilla ya Spain Jorge Sampaoli anatajwa kushika wadhifa huu.