Saturday, April 15, 2017

CAF CONFEDERATION CUP: LEO NI MC ALGER vs YANGA, TAMBWE KUANZIA BENCHI!

MABINGWA wa Tanzania Bara Yanga Leo wapo huko Agiers, Algeria kuivaa Mouloudia Club d'Alger wakitakiwa kulinda ushindi wao wa 1-0 walioupata Jijijni Dar es Salaam Wiki iliyopita ili kutinga Hatua ya Makundi ya Mashindano ya CAF Kombe la Shirikisho.
Yanga wanahitaji Sare yoyote au hata wakifungwa kwa kiasi cha 2-1, 3-2, 4-3 au kifungo chochote cha Magoli cha tofauti ya Bao moja, basi watafuzu.

Kwenye Mechi ya Leo Yanga itawakosa Obrey Chirwa, Vincent Bossou na Oscar Joshua ambao hawakwenda huko Algreria walikotua Jana. Mechi hii itachezeshwa na Refa Yakhouba Keita kutoka Guinea.