Saturday, April 22, 2017

FA CUP: CHELSEA 4 VS 2 tottenham hotspur

Nusu Fainali ya FA CUP imechezwa huko London Uwanja wa Wembley kati ya Chelsea na Tottenham Hotspur Timu ambazo kwenye EPL, Ligi Kuu England zipo Nafasi za Kwanza na za Pili na Mshindi kuibuka ni Chelsea kwa Bao 4-2.
Chelsea ndio waliotangulia kufunga katika Dakika ya 5 kwa Frikiki ya Willian na Spurs kusawazisha Dakika ya 18 baada ya Krosi ya Eriksen kuparazwa kwa Kichwa na Harry Kane na kutinga Wavuni.

Chelsea walikwenda 2-1 mbele katika Dakika ya 42 kwa Penati ambayo Mshika Kibendera kuashiria kuwa Son Heung-min alimwangusha Victory Moses na Refa Martin Atkinson kumkubalia na Penati hiyo kufungwa na Willian.
Hadi Haftaimu, Chelsea 2 Spurs 1.

JE WAJUA?
-FA CUP 2016/17, ambalo pia hujulikana kama FA Challenge Cup, ni mara ya 136 kushindaniwa kila Mwaka tangu lilipoanzishwe na linatambuliwa kama ndio Mashindano ya kale kupita yote Duniani.

-Kombe hili linadhaminiwa na Kampuni ya Ndege ya Emirates na kwa sababu za kiudhamini linaitwa Emirates FA Cup.

-Timu 736 zilikubaliwa kushiriki Mashindano haya Msimu huu na yalianza kwa Raundi ya Awali na yatafikia Tamati kwa Fainali itakayochezwa Uwanjani Wembley Jijini London hapo Mei 27, 2017.
-Mshindi wa FA CUP ataingizwa Hatua ya Makundi ya UEFA EUROPA LIGI Msimu wa 2017/18.


KUANZIA MSIMU HUU – KUANZIA Robo Fainali:
-Hamna Marudiano ikiwa Timu zipo Sare baada ya Dakika 90. Sare itafuatia Dakika za Nyongeza 30 na kama Gemu bado Sare, zitafuatia Penati ili kupata Mshindi.

-Kila Timu inaruhusiwa kubadili Wachezaji si zaidi ya Wanne lakini huyo wa Nne ni pale tu Gemu ipo Dakika za Nyonfeza 30.


Kipindi cha Pili Dakika ya 52, Pasi yenye akili ya Eriksen ilimkuta Dele Alli ndani ya Boksi na akamilizia vizuri na kuipa Sare Spurs.

Dakika ya 61, Antonio Conte alifanya mabadiliko Mawili kwa Mpigo kwa kuwatoa Willian na Batshuayi na kuwaingiza Eden Hazard na Diego Costa.
Eden Hazard aliifungia Chelsea Bao la 3 Dakika ya 75 alipofyatua Mkwaju nje ya Boksi kufuatia Kona iliyookolewa na Chelsea kwenda 4-2 mbele kwa kigongo kingine kikali cha Mita 25 cha Nemanja Matic.
Nusu Fainali ya Pili ya FA CUP itachezwa Kesho Jumapili pia Uwanjani Wembley kati ya Arsenal na Manchester City.

VIKOSI:
CHELSEA:
Courtois, Azpilicueta, Luiz, Ake, Moses, Kante, Matic, Alonso, Willian [Eden Hazard, 61], Batshuayi [Diego Costa, 61], Pedro [Fabregas, 73]
Akiba: Begovic, Zouma, Terry, Chalobah, Fabregas, Hazard, Costa.

TOTTENHAM HOTSPUR: Lloris, Trippier, Dier, Alderweireld, Vertonghen, Wanyama [Nkoudou, 79], Dembele, Son [Walker, 68], Eriksen, Dele, Kane.
Akiba: Lopez, Davies, Walker, Wimmer, Sissoko, Nkoudou, Janssen.
REFA: Martin Atkinson

Chelsea BAO zake zimefungwa na

Willian (5', 43' PEN)
Eden Hazard (75')
Nemanja Matic (80')


Tottenham Hotspur bao zake zilifungwa na 
Harry Kane (18')
Dele Alli (52')