Thursday, April 20, 2017

DROO MECHI ZA NUSU FAINALI UEFA CHAMPIONS LIGI NA EUROPA LIGI IJUMAA!

DROO za kupanga Mechi za Mashindano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, na UEFA EUROPA LIGI zitafanyika Ijumaa Aprili 21 huko Nyon, Uswisi kwenye Makao Makuu ya UEFA.
Tayari Timu zilizotinga Nusu Fainali za UCL zilikamilka hapo Jana wakati 4 za EUROPA LIGI zitajulikana baadae Usiku wa Leo baada kukamilika Mechi 4 za Pili za Robo Fainali.
Kwenye Mechi hizo za Robo Fainali Man United watacheza na RSC Anderlecht (Mechi ya Kwanza 1-1), KRC Genk kuivaa Celta Vigo (2-3), Schalke na Ajax (0-2) na Besiktas kucheza na Lyon (1-2).

Kwenye Chungu cha Droo ya UCL Timu 4 ambazo zimo humo ni Mabingwa Watetezi Real Madrid, Atletico Madrid, Juventus na AS Monaco.
Droo hii haibagui Timu za Nchi moja na hivyo upo uwezekano wa kuwepo El Derbi Madrileno kwa Mahasimu Real na Atletico kupambanishwa.
Droo hizi 2, zile za UCL na EUROPA LIGI, zitaanza Saa 7 Mchana.
Mechi za Nusu Fainali za UCL zitachezwa Mei 2 na 3 na Marudiano Wiki 1 baadae hapo Mei 9 na 10 huku Fainali ikichezwa Cardiff, Wales Juni 3.
Mechi za Nusu Fainali za EUROPA LIGI zitachezwa Alhamisi Mei 4 na kurudiana ni Mei 11.
Fainali ni huko Stockholm, Sweden hapo Mei 24.