Friday, April 21, 2017

DROO YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE YATOKA! REAL MADRID vs ATLETICO MADRID, AS MONACO vs JUVENTUS

DROO za Mashindano makubwa ya Klabu Ulaya zimefanyika Mchana huu huko Nyon, Uswisi Makao Makuu ya UEFA na Manchester United kupambanishwa na Celta Vigo ya Spain katika Nusu Fainali ya UEFA EUROPA LIGI.

Kwenye Droo za UEFA EUROPA LIGI, Mabingwa Watetezi Real Madrid wamekutanishwa na Mahasimu wao Wakuu wa Jiji la Madrid Nchini Spain Atletico Madrid Mechi ambayo ina Ubatizo wa Jina la ‘El Derbi Madrileno’!
Mechi nyingine za Nusu Fainali ni Ajax ya Netherlands dhidi ya Lyon ya France kwenye EUROPA LIGI na AS Monaco kucheza na Juventus katika UEFA CHAMPIONS LIGI.
Man United wametwaa Ubingwa wa Ulaya mara 3 lakini hawajawahi kubeba Kombe hili ambalo ni la Pili kwa ukubwa huko Ulaya.
Lakini Meneja wa sasa Man United, Jose Mourinho, aliwahi kutwaa Kombe hili akiwa na Klabu ya Ureno FC Porto Mwaka 2003 na wanakutana na Celta Vigo ambayo haijawahi kutwaa Kombe lolote Ulaya.
Mechi za Kwanza za Nusu Fainali za EUROPA LIGI zitachezwa Mei 4 na Marudiano ni Mei 11 wakati Fainali itakuwa Stockholm, Sweden hapo Mei 24.
Kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI, Real wanasaka kutetea Ubingwa wao na kuwa Klabu ya kwanza kuweka Historia hiyo.
Mechi zao za Nusu Fainali zitachezwa Mei 2 na 3 na Marudiano Wiki Moja baadae huku Fainali ikichezwa Juni 3 huko Cardiff, Wales.
Atletico wanaweza kuwafunga na kuwapoteza Real Madrid kwenye Uefa Champions League.UEFA CHAMPIONS LEAGUE
SEMIFINAL DRAW:
The first legs will take place on May 2 and 3, with the second legs the following week.

Real MadridvsAtletico Madrid
Monaco vsJuventus