Tuesday, April 18, 2017

ENGLAND: SPURS, CHELSEA KWENYE PATASHIKA YA KUUTAFUTA UBINGWA! MECHI 6 TU ZIMEBAKI.

Wikiendi hii iliyopita Tottenham iliichapa Bournemouth 4-0 na Chelsea kuchapwa 2-0 na Manchester United na kuzifungua mbio za Ubingwa wa England za EPL, Ligi Kuu England.
Ingawa kimahesabu Timu kadhaa ambazo zipo juu kwenye Msimamo wa Ligi zinaweza kuutwaa Ubingwa lakini Wachambuzi wanazipa nafasi kubwa Vinara Chelsea na Timu ya Pili Tottenham maarufu kama Spurs.
Zikiwa zimebakisha Mechi 6 kila mmoja, Chelsea ndio wapo kileleni wakiwa na Pointi 75 na kufuatia Spurs wenye Pointi 71.

Wikiendi hii Chelsea na Spurs zitapambana kwenye Uwanja wa Wembley Jijini London kwenye Mechi ya Nusu Fainali ya FA CUP Mechi ambayo inasemwa itatoa morali kwa Mshindi kuelekea Ubingwa.
Kwa Mechi 6 zilizobaki kwa Timu hizi mbili, Spurs ndio wanaonekana kuwa na Ratiba ngumu kupita Chelsea kwani wanapaswa kuzivaa Arsenal, Man United na Mabingwa Leicester City miongoni mwa Mechi zao wakati Chelsea, kimtazamo, Mechi yao ngumu ni dhidi ya Everton tu.

EPL, Ligi Kuu England – Mechi zilizobaki:
-U=Ugenini N=Nyumbani
Tottenham – RATIBA:

Aprili 22: Chelsea [FA Cup Nusu Fainali, Wembley]
Aprili 26: Crystal Palace [U]
Aprili 30: Arsenal [N]
Mei 6: West Ham United [U]
Mei 13: Man United [N]
Mei 18: Leicester [U]
Mei 21: Hull City [U]

CHELSEA – RATIBA:
Aprili 22: Tottenham [FA Cup Nusu Fainali, Wembley]
Aprili 25: Southampton [N]
Aprili 30: Everton [U]
Mei 8: Middlesbrough [N]
Mei 12: West Brom [U]
Mei 15: Watford [N]
Mei 21: Sunderland [N]