Sunday, April 2, 2017

FULL TIME: ARSENAL 2 v 2 MANCHESTER CITY


Arsenal wakiwa kwao Emirates ambako baadhi ya Mashabiki kwa mara nyingine walileta shinikizo ili Meneja Arsene Wenger ang’oke, Arsenal mara mbili walitoka nyuma na kuambua Sare ya 2-2 walipocheza na Manchester City na kubakia Nafasi ya 6 kwenye EPL, Ligi Kuu England.
City walitangulia kufunga Dakika ya 5 tu kupitia Leroy Sane na Arsenal kusawazisha Dakika ya 40 kwa Bao la Theo Walcott lakini Dakika 2 baadae City wakenda 2-1 mbele kwa Goli la Sergio Aguero.
Dakika ya 53 Beki Shkodran Mustafi akaikomboa Arsenal kwa Bao la Kichwa alipounganisha Kona ya Mesut Ozil na kuwapa Arsenal Pointi 1.
Sare imewaacha City Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 5 mbele ya Timu ya 5 Man United wenye Mechi 1 mkononi na Arsenal wapo Nafasi ya 6 Pointi 2 nyuma ya Man United.
EPL itarindima tena Jumanne na Jumatano kwa Timu zote 20 kuwa dimbani na Bigi Mechi, bila shaka, ipo Jumatano Stamford Bridge wakati Vinara Chelsea wakiivaa Man City.
VIKOSI:
ARSENAL:
Ospina, Bellerin, Mustafi, Koscielny [Gabriel 45’], Monreal, Xhaka, Coquelin, Walcott [Giroud 68'], Ozil, Welbeck [Iwobi 77'], Sanchez
Akiba: Gibbs, Gabriel, Giroud, Iwobi, Martinez, Elneny, Maitland-Niles.
MAN CITY: Caballero, Fernandinho, Stones, Otamendi, Clichy, Jesus Navas, De Bruyne, Silva [Zabaleta 89'], Sane, Sterling [Touré 45'], Aguero
Akiba: Bravo, Kompany, Zabaleta, Nolito, Kolarov, Delph, Toure.