Saturday, April 1, 2017

FULL TIME: LIVERPOOL 3 vs 1 EVERTON

BAO za Liverpool zilifungwa na
Sadio Mané dakika ya 8
Philippe Coutinho dakika ya 31
Divock Origi ya 60 kipindi cha pili.
Bao la kufutia machozi la Everton limefungwa na
Matthew Pennington kipindi cha kwanza dakika ya 28.

Mtanange wa Jiji la Liverpool, maarufu kama Dabi ya Merseyside, ulichezwa Leo Uwanja wa Anfield na Liverpool kuichapa Everton 3-1.
Dakika ya 8 Liverpool walipata Bao kwa uhodari binafsi wa Straika kutoka Senegal Sadio Mane ambae alipokea Pasi toka Mstari wa Kati ya Uwanja na kuchanja mbuga na kuingia ndani ya Boksi na kuachia Shuti la chinchini liliowapita Mabeki kadhaa na kutinga wavuni.

Dakika ya 28 kizaazaa cha Kona ya Everton kiliufanya Mpira umdondokee Matthew Pennington, aliekuwa akicheza Mechi yake ya kwanza Msimu huu, na kuisawazishia Everton.
Dakika 3 baadae umahiri wa Philippe Coutimho uliipa Liverpool Bao la Pili alipowahadaa Mabeki kadhaa na kuachia Shuti safi hadi wavuni.
Hadi Mapumziko, Liverpool 2 Everton 1.
Kwenye Dakika ya 56 Liverpool wakalazimika kumtoa Sadio Mane alieumia na nafasi yake kuchukuliwa na Divock Origi ambae Dakika 4 baadae akaifungia Liverpool Bao la 3. 


VIKOSI:
LIVERPOOL: Mignolet, Clyne, Matip, Lovren, Milner, Can, Lucas, Wijnaldum, Mane [Origi, 56], Firmino (Klavan, 90), Coutinho (Alexander-Arnold, 74)
Akiba: Karius, Grujic, Klavan, Moreno, Origi, Woodburn, Alexander-Arnold.
EVERTON:Robles, Jagielka, Williams, Holgate, Pennington (Barry, 67), Davies (Valencia, 66), Gueye, Baines, Barkley, Lukaku, Calvert-Lewin (Mirallas, 82)
Akiba: Kone, Mirallas, Barry, Valencia, Stekelenburg, Lookman, Kenny.
REFA: Anthony Taylor