Thursday, April 6, 2017

JESSE LINGARD ASAINI MIAKA 4 MANCHESTER UNITED, AFURAHIA DILI HILO NA KUSEMA MOYO WAKE NI MAN UNITED

JESSE LINGARD anasemekana atapewa Dili mpya Klabuni kwake Manchester United ya Mkataba wa Miaka Minne na Mshahara wake kuongezeka mara 3 na kuvuna zaidi ya £100,000 kwa Wiki.

Lingard amebakiza Mwaka Mmoja kwenye Mkataba wake wa hivi sasa na Man United wamekuwa wakitaka abakie kwa muda mrefu zaidi.
Fowadi huyo mwenye Miaka 24 yupo Man United tangu akiwa na Umri wa Miaka 7 na alipewa Mkataba wake wa kwanza kama Profeshenali Mwaka 2011.
Lingard alianza kuchomoza na kubaki Timu ya Kwanza Msimu uliopita chini ya Meneja Louis van Gaal na kabla ya hapo alipelekwa kwa mkopo kwenye Klabu za Leicester City, Birmingham City, Brighton na Derby County.

Kabla habari hizi kuibuka Lingard, ambae ameanza Mechi 3 zilizopita za Man United, alithibitisha yupo mazungumzoni kuongeza Mkataba wake huku yeye akisisitiza angependelea kubakia hapo hapo.
Alieleza: “Nafurahia kuichezea Man United na Moyo wangu ni Man United!”
Lingard amebainisha kuna ushindani mkali kwenye Timu kupata namba lakini pia amekiri hilo ni jambo jema kwa Timu ambalo linakufanya ukipata nafasi basi lazima ujitume.

Amesema: “Ukiwaangalia Mkhitaryan, Zlatan, Pogba, ni Majina makubwa kwenye Timu yetu na ni vyema kuwaiga kwa yale waliyofanikiwa na ni wazi tunapata uzoefu toka kwao hasa kwa Wachezaji Chipukizi!”