Sunday, April 16, 2017

JOSE MOURINHO AIPIMIA CHELSEA KULIPA KISASI!

EPL, LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Jumapili Aprili 16

15:30 West Bromwich Albion v Liverpool
18:00 Manchester United v Chelsea

LEO EPL, Ligi Kuu England, ina Mechi kali huko Old Trafford Jijini Manchester kati ya Wenyeji Manchester United na Vinara wa Ligi hii Chelsea.
Mapema Msimu huu, Chelsea iliifunga Man United 4-0 huko Stamford Bridge kwenye Mechi ya EPL lakini kwenye Mechi kama hii ya Ligi Msimu uliopita Timu hizi zilitoka 0-0 Uwanjani Old Trafford.
Mbali ya Mechi hii kukutanisha Timu Vigogo, pia inamkutanisha Jose Mourinho, Meneja wa Man United, dhidi ya Klabu yake ya zamani Chelsea ambayo sasa ipo chini ya Mtaliana Antonio Conte huu ukiwa Msimu wake wa kwanza.
Chelsea hivi sasa wapo kileleni mwa EPL wakiwa Pointi 4 mbele ya Tottenham ambao Jana waliitwanga Bournemouth 4-0 na kuikaribia Chelsea ingawa wamecheza Mechi 1 zaidi.
Wakati Chelsea wakiwa Mapumzikoni kwa Wiki nzima wakiingoja Man United na bila kuwa na Majeruhi kwenye Kikosi chao, Man United Alhamisi Usiku walikuwa huko Belgium kucheza Mechi ya Robo Fainali ya UEFA EUROPA LIGI ambayo walitoka 1-1 na RSC Anderlecht.
Pia, Man United wana Majeruhi kadhaa ambao ni Ashley Young, Phil Jones, Chris Smalling na Juan Mata huku Nahodha wao Wayne Rooney akiwa na hatihati kucheza kutokana na maumivu.


KUKUTANA: USO KWA USO
Man United: Ushindi 75
Chelsea: Ushindi 52
Sare: 49