Saturday, April 22, 2017

KUMEKUCHA EL CLASICO, REAL MADRID vs BARCELONA

JUMAPILI KESHO ESTADIO SANTIAGO BERNABEU itafurika kwa mtanange unaobatizwa EL CLASICO kati ya Real Madrid na Barcelona.
Siku zote pambano hili ni muhimu lakini safari hii muhimu zaidi kwani Real sasa wanaongoza La Liga wakiwa na Pointi 75 kwa Mechi 31 na Barcelona ni wa Pili wakiwa na Pointi 72 kwa Mechi 32.
Ushindi kwa Real utawafanya wawe Pointi 6 mbele ya Barca na Mechi 1 mkononi huku Mechi zikibaki 6 kwa Real na 5 kwa Barca.


Real ambao hawajatwaa Ubingwa wa La Liga tangu 2012 watatakiwa kushinda hii El Clasico na kisha Mechi zao 3 zilizobaki ili kuubeba Ubingwa.
Kipigo kwa Barca kitafuta kabisa matumaini yao ya Ubingwa.
Kwenye Mechi yao ya Kwanza ya La Liga Msimu huu iliyochezwa huko Nou Camp, Barcelona na Real Madrid zilitoka Sare 1-1 hapo Desemba 3.
Luis Suarez ndie alieipa Bao Barca katika Dakika ya 53 na Sergio Ramos kusawazisha Dakika ya 90.