Tuesday, April 4, 2017

LIVERPOOL KWENYE WASIWASI WA KUMKOSA SADIO MANE MSIMU HUU

Liverpool wapo kwenye hofu kubwa juu ya Sadio Mane kutocheza tena Msimu huu uliobaki baada ya Jumamosi kuumia Goti kwenye Mechi waliyowachapa Everton 3-1.
Fowadi huyo kutoka Senegal ambae ndie tegemeze kubwa la Liverpool na ambae ndie aliewafungia Bao la Kwanza kwenye Mechi hiyo na Everton aliumia baada kuvaana na Leighton Baines wa Everton.

Image result for sadio maneBaada ya Mechi hiyo ya Jumamosi, licha mwenyewe Mane kusisitiza yuko fiti kwa Mechi yao ya Jumatano dhidi ya Bournemouth, Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema hataweza kucheza Mechi ijayo.
Mane anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kina baada uvimbe kupungua kwenye Goti lake lakini upo wasiwasi mkubwa huenda asionekane tena hivi karibuni.
Fowadi huyo anaungana na Majeruhi wengine Jordan Henderson na Adam Lallana ambao wamepelekwa.huko USA kwa matibabu zaidi.

Mchezaji mwingine alieumia kwenye Mechi hiyo na Everton ni Kiungo Emre Can ambae ameshindwa kufanya hata Mazoezi kutokana na maumivu ya Goti.
Lakini habari njema kwa Liverpool ni kuanza tena Mazoezi kwa Straika wao Daniel Sturridge ambae kitambo yuko nje kwa maumivu na upo uwezekano akawepo Benchi Jumatano wakiivaa Bournemouth.