Monday, April 3, 2017

MOURINHO AWASHUKIA MASTAA WAKE AKIWEMO DOGO SHAW

MENEJA wa Manchester United Jose Mourinho amehoji anavyojituma Luke Shaw kwa Klabu hiyo.
Shaw, Fulbeki wa Kushoto mwenye Miaka 21, ameichezea Man United mara 15 Msimu huu na hajaonekana Uwanjani tangu walipotoka 1-1 na Bournemouth Mwezi uliopita.


Mourinho amedai Shaw hawezi kulinganishwa vizuri na Mabeki wengine kama kina Ashley Young, Matteo Darmian na Daley Blind.
Mourinho amefunguka: “Siwezi kulinganisha jinsi anavyofanya Mazoezi, anavyojituma, mkazo na nia yake. Yuko nyuma mno!”

Mourinho alihojiwa kama Shaw, Mchezaji wa Kimataifa wa England, anahitaji kujisukuma zaidi na akajibu: “Joe Hart ni Mchezaji wa Kimataifa wa England na yupo kwa Mkopo Italy!”

Shaw alijiunga na Man United Juni 2014 kwa Dau la Pauni Milioni 27 na Septemba 2015 alivunjika Mguu wake sehemu 2 na kuwa nje kwa karibu Mwaka mzima.
Mwezi Novemba, Mourinho alimponda Beki huyo aliesema hayuko tayari kucheza Mechi ya Ligi dhidi ya Swansea City.