Tuesday, April 18, 2017

NAHODHA JOHN TERRY AAGA CHELSEA, MWENYEWE NA KLABU ZATHIBITISHA!

NAHODHA wa Chelsea John Terry ataondoka Klabuni hapo baada ya kudumu kwa Miaka 20.
Mkataba wa Terry ulimalizika Mwaka Jana na akapewa Nyongeza ya Mwaka Mmoja Mwezi Mei 2016.
Terry, mwenye Miaka 36, pamoja na Chelsea, zimethibitisha kung’atuka kwa Mchezaji huyo ambae ndie ametwaa Mataji mengi kupita Mchezaji yeyote katika Historia ya Klabu hiyo.
Terry ameshinda Ubingwa wa England mara 4, UEFA CHAMPIONS LIGI 1, FA CUP 5, EUROPA LIGI 1 na Kombe la Ligi mara 3.
Alianza kuichezea Chelsea kwa mara ya kwanza 1998 na kucheza Mechi 713 na kati ya hizo 578 kama Nahodha.
Terry ameeleza: “Najisikia bado naweza kucheza lakini hapa Chelsea sitapata nafasi nyingi!”

Terry, ambae ni Sentahafu, amefunga Bao 66 akiwa na Chelsea alikoanza kucheza akiwa na Miaka 14 lakini Msimu huu ameanza Mechi 4 tu za EPL, Ligi Kuu England.
Beki huyo ndie anaeshika nafasi ya 3 kwa kucheza Mechi nyingi hapo Chelsea katika Historia akiwa nyuma ya Ron Harris na Peter Bonetti.
Terry alistaafu kuichezea Timu ya Taifa ya England Mwaka 2012 alipoichezea Mechi 78.