Wednesday, April 26, 2017

NEWCASTLE YAFURAHIA KURUDI LIGI KUU ENGLAND

NEWCASTLE UNITED Jana ilifanikiwa kurejea EPL, Ligi Kuu England, baada ya Msimu mmoja kwenye Daraja la chini, Championship, walipoifunga Mtu 10 Preston North End 4-1 huko Saint James Park.
Bao za Newcastle, ambao waliongoza 2-1 hadi Haftaimu, zilifungwa na Ayoze Perez, Bao 2, Christian Atsu na Matt Ritchie [Penati baada ya Paul Gallagher kushika Mpira kwenye Mstari wa Goli na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu].

Newcastle, chini ya Meneja Rafael Benitez, wanaungana na Brighton kutinga moja kwa moja EPL na kubakiza Nafasi 1 itayogombewa na Timu zitakazomaliza Nafasi za 3, 4, 5 na 6.

https://images.nufc.co.uk/900x506_/media/30329/christian-atsu-preston-goal.jpgHuku zikibaki Mechi 2, Brighton ndio wanaongoza Championship wakiwa na Pointi 92 wakifuata Newcastle wenye 88.
Nafasi za 3 hadi za 6 zinashikwa na Reading, 79, Sheffield Wednesday, 78, Huddersfield, 78, na Fulham, 76.
Leeds United, ambao wako Nafasi ya 7 wakiwa na Pointi 73, wanaweza pia kuingia Kundi hilo la Mechi za Mchujo.
Kikosi cha Rafael Benitez kimekuwa kikisuasua katika Mechi zao za hivi karibuni kwa kambua Pointi 1 tu katika Mechi 3 zilizopita lakini ushindi wa Jana ulipokewa kwa furaha kubwa na Mashabiki 50,000 waliorundika Saint James Park.