Wednesday, April 26, 2017

N'GOLO KANTE AZOA TUZO YA PFA, NDIE BORA ENGLAND, DELE ALLI BORA KWA VIJANA MSIMU WA PILI MFULULIZO!

KIUNGO wa Chelsea N'Golo Kante amezoa Tuzo ya Mchezaji Bora kwa Msimu wa 2016/17 inayotolewa na PFA ( Professional Footballers Association), Chama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa huko England.
Kiungo huyo wa Chelsea wa Miaka 26 anaetoka France aliwabwaga Eden Hazard, Harry Kane, Romelu Lukaku, Zlatan Ibrahimovic na Alexis Sanchez katika Kura iliyopigwa na Wachezaji wenzake wa Kulipwa.
Kwenye Tuzo ya Mchezaji Kijana Dele Alli wa Tottenham Hotspur ameizoa tena kwa Msimu wa Pili mfululizo.
Akiongelea ushindi wa Tuzo hii, Kante alisema: "Ni heshima kubwa mno kuchaguliwa na Wachezaji wengine!"


MJUE KANTE:
KUZALIWA: Paris, France
UMRI: Miaka 26
KLABU ALIZOCHEZA: Boulogne (2011-13), Caen (2013-15), Leicester (2015-16), Chelsea (2016-)
MATAJI: EPL 2015/16Hivi sasa Kante yuko mbioni kutwaa Ubingwa wa England akiwa na Chelsea ambao ndio Vinara wa EPL, Ligi Kuu England, baada ya Msimu uliopita kutwaa Ubingwa huo akiwa na Leicester City.Kante anaweza kuweka Rekodi ya kuwa Mchezaji wa Kwanza kutwaa Ubingwa wa England Misimu Miwili mfululizo akiwa na Klabu Mbili tofauti ikiwa Chelsea itafanya vyema Mechi zake 6 zilizobaki.