Saturday, April 15, 2017

POGBA AJITETEA! ASEMA ‘MSINIHUKUMU KWA ADA YA UHAMISHO AU MAGOLI!’

Paul Pogba amesema asihukumiwe kwa Kiwango cha Ada yake ya Uhamisho au Magoli anayofunga kwani yupo wakati murua Klabuni Manchester United.
Pogba, ambae alivunja Rekodi ya Ada ya Uhamisho Duniani alipohama kutoka Juventus mwanzoni mwa Msimu huu, amesema anaamini anaandamwa pasipo na haki licha ya kuisaidia Man United kubeba EFL CUP pamoja na Ngao ya Jamii na bado wapo mawindoni kutwaa UEFA EUROPA LIGI.
Akiongea na Wanahabari kuelekea Mechi yao ya Robo Fainali ya huko Brussells, Belgium dhidi ya RSC Anderlecht ikiwa ni Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya UEFA EUROPA LIGI, Pogba amejieleza vizuri tu.

Amesema: “Najisikia safi, kwa kweli. Tumetwaa Vikombe Viwili, lakini ni wazi nataka kufanya vyema zaidi. Nafanya vizuri, Timu ipo vizuri na tunatilia mkazo kubeba EUROPA LIGI na kupigania 4 Bora kwenye Ligi. Mie nimesahau Ada ya Uhamisho, hiyo imepita, naangalia Uwanjani na kufanya vyema kwa Timu yangu.”

Ameongeza: “Watu wanataka nifunge Magoli na wananihukumu kwa kutofunga Magoli, lakini hiyo ndio Soka. Wanataka nifunge kwa sababu ya Ada ya Uhamisho. Kazi yangu ni Kiungo, kutengeneza Mabao. Kama ningefunga yale Magoli yote yaliyopiga Posti [Mashuti 9], Watu wangekuwa kimya!”
Alipoulizwa tofauti ya Soka la Italy na England na hasa hii mara ya pili kucheza England, Pogba alijibu: “Huko Italy ni mbinu, Magoli machache. Lakini hapa England, ni kushambulia na ni ngumu. Timu 5 za juu na zile 2 za juu zinakaribiana mno. Hujui nini litatokea…tizama Arsenal kapigwa 3-0 na Crystal Palace!”

EPL, LIGI KUU ENGLAND
RATIBA

Jumamosi Aprili 15
1430 Tottenham Hotspur v Bournemouth
1700 Crystal Palace v Leicester City
1700 Everton v Burnley
1700 Stoke City v Hull City
1700 Sunderland v West Ham United
1700 Watford v Swansea City
1930 Southampton v Manchester City

Jumapili Aprili 16
1530 West Bromwich Albion v Liverpool
1800 Manchester United v Chelsea

Jumatatu
2200 Middlesbrough v Arsenal