Saturday, April 29, 2017

RASMI: MOYES NA SUNDERLAND YAKE YASHUKA DARAJA

Sunderland news: Black Cats RELEGATED from Premier LeagueLEO Sunderland wameiaga rasmi EPL, Ligi Kuu England, baada ya kufungwa 1-0 na Bournemouth Uwanjani Stadium of Light.
Matoke ohayo na ile Sare ya Southamton na Hull City ndio yamemaliza Miaka 10 ya Sunderland kubakia EPL.
Bao la ushindi la Bournemouth lilifungwa Dakika ya 88 na Joshua King.
Nao Leicester City wamepata ushindi wa Ugenini wa 1-0 dhidi ya West Bromwich Albion kwa Bao la Jamie Vardy.
Baadae Leo, huko Selhurst Park Jijini London, Crystal Palace watacheza na Burnley.

EPL itaendelea tena Jumapili kwa Mechi 4 na ya mwanzo kabisa ni huko Old Trafford ambako Manchester United watacheza na Swansea City na Usiku kumalizika kwa Mechi kali huko White Hart Lane katika Dabi ya London ya Kaskazini kati ya Tottenham Hotspur na Arsenal.
Kati ya Mechi hizo, Vinara Chelsea watakuwa Ugenini huko Goodison Park Jijini Liverpool kuivaa Timu ngumu Everton.

Mechi nyingine hiyo Jumapili ni huko Riverside ambapo Middlesbrough watacheza na Man City.