Saturday, April 8, 2017

REAL MADRID 1 - 1 ATLETICO MADRID,GRIEZMAN HATARI SANA! HAINYIMA REAL USHINDI

BAO la Antoine Griezmann zikiwa zimesalia Dakika 5 Mpira kwisha limeipa Atletico Madrid Sare ya 1-1 walipocheza na Real Madrid Uwanjani Santiago Bernabeu kwenye Mechi ya La Liga ambayo ni maarufu kama El Derbi Madrileno.
Real walitangulia kufunga Dakika ya 52 kwa Kichwa cha Pepe alieunganisha Frikiki.
Matokeo haya bado yamewaweka Real Pointi 3 mbele ya Barcelona huku wote wakiwa wamecheza Mechi 30 na kubakisha 8.
Aprli 23 Real wataivaa Barcelona Uwanjani Santiago Bernabeu.

VIKOSI:
Real Madrid (Mfumo 4-3-3):
Navas; Dani Carvajal, Pepe, Sergio Ramos, Marcelo; Modric, Casemiro, Kroos; Bale, Benzema, Ronaldo.
Akiba: Nacho, James, Kiko Casilla, Kovacic, Lucas Vazquez, Alvaro Morata, Isco.

Atletico Madrid (Mfumo 4-4-2):
Oblak; Juanfran, Savic, Godin, Filipe Luis; Carrasco, Saul, Gabi, Koke; Torres, Griezmann.
Akiba: Correa, Cerci, Lucas, Partey, Gimenez, Andre Moreira, Roberto Nunez.