Friday, April 7, 2017

SADIO MANE NJE MSIMU WOTE 2016/2017, KLOPP ATAKA WACHEZAJI WAKE KUKAZA WALIPO!

Liverpool wamethibitisha kuwa Fowadi wao Sadio Mane hatocheza tena Msimu huu uliobaki baada ya Jumamosi iliyopita kuumia Goti kwenye Mechi waliyowachapa Everton 3-1.

Fowadi huyo kutoka Senegal mwenye Miaka 24 na ambae ndie tegemeze kubwa la Liverpool na ambae ndie aliewafungia Bao la Kwanza kwenye Mechi hiyo na Everton aliumia baada kuvaana na Leighton Baines wa Everton.

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema ana hakika Mane anahitaji upasuaji na itakuwa ngumu kwake kucheza tena Msimu huu unaokwisha Mwezi ujao.
Mane, aliesainiwa kutoka Southampton kwa Dau la Pauni Milioni 34, amecheza Mechi zote za Liverpool Msimu huu kasoro 5 tu.
Kati ya Mechi hizo, 3 zilikuwa Sare na 2 wamefungwa na kuwaacha Liverpool wakiwa Nafasi ya 3 kwenye EPL, Ligi Kuu England, wakiwa na Pointi 60 kwa Mechi 31 wakiwa Pointi 12 nyuma ya Vinara Chelsea.

Fowadi huyo anaungana na Majeruhi wengine Jordan Henderson na Adam Lallana ambao wamepelekwa huko USA kwa matibabu zaidi.
Mchezaji mwingine alieumia kwenye Mechi hiyo na Everton ni Kiungo Emre Can ambae ameshindwa kufanya hata Mazoezi kutokana na maumivu ya Goti.
Lakini habari njema kwa Liverpool ni kuanza tena Mazoezi kwa Straika wao Daniel Sturridge ambae kitambo yuko nje kwa maumivu na upo uwezekano akawepo Benchi Jumatano wakiivaa Bournemouth.
Jurgen Klopp's Liverpool have posted great performances against top teams, but struggled against lesser sides. How can he bring more consistency to his team?