Tuesday, April 4, 2017

SIKU CHACHE BAADA YA KUIBAMIZA SIMBA KAITABA, MBARAKA YUSUPH MCHEZAJI BORA WA LIGI MWEZI MACHI, 2017


Mchezaji Chipukizi wa Kagera Sugar Mbaraka Yusuph ameibuka mchezaji bora wa LIGI Kuu Vodacom mwezi Machi, 2017 ni siku chache tu baada ya kuonesha kiwango na nidhamu kubwa katika mchezo ambao aliifungia bao moja Timu ya kagera Sugar dhidi yaSimba siku ya Jumapili. Kagera walishinda bao 2-1 kwenye Uwanja wa Kaitaba juzi jumapili. Mbaraka Yusuph atapokea kitita cha Millioni 1 kutoka wadhamini wa Vodacom Tanzania. Hii ni baada ya miezi michache kama mitatu kupita baada ya pia mchezaji Mlinda mlango Juma Kaseja kuibuka mchezaji bora wa mwezi Januari 2017.

Mchezaji wa timu ya Kagera Sugar FC, Mbaraka Yusuph Abeid amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Machi kwa msimu wa 2016/2017.
Mbaraka aliwashinda wachezaji Abubakar Salum wa Azam FC na Kenny Ally wa Mbeya City kutokana na kuonyesha kiwango cha hali ya juu, hivyo kuisadia timu yake kupata matokeo mazuri.